TRT Afrika Swahili
banner
sw.trtafrika.com
TRT Afrika Swahili
@sw.trtafrika.com
Afrika kama ilivyo
Je, unazikumbuka nukuu hizi zilizogonga vichwa vya habari kwa mwaka 2024?
December 24, 2024 at 8:53 AM
Rais wa Kenya William Ruto atoa zawadi za Krismasi kwa watoto wasiojiweza. Rais Ruto ametoa zawadi aina mbalimbali ikiwemo chakula katika vituo vya kulelea watoto katika kaunti ya Uasin Gishu na kitongoji chake
December 24, 2024 at 8:37 AM
Olimpiki ya Maasai 2024 iliyofanyika Kimana, Kajiado Kenya, yenye lengo la kuwapa shughuli mbadala kuliko kuua simba
December 18, 2024 at 7:54 AM
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban katika Ikulu ya Ankara
December 12, 2024 at 12:24 PM
Rais William Ruto wa Kenya ametuma salamu za pongezi kwa Wakenya wakati taifa hilo linaposherehekea miaka 61 tangu kuwa Jamhuri.

Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa jijini Nairobi katika viwanja vya Uhuru Gardens na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.
December 12, 2024 at 11:51 AM
Kenya imeadhimisha miaka 61 tangu kuwa Jamhuri, 12 Desemba 1963 baada ya kupata utawala wa ndani mnamo 1 Juni 1963 (Siku ya Madaraka) kutoka Muingereza.
December 12, 2024 at 11:37 AM
Siku ya Disemba 12, Kenya inaaadhimisha miaka 61 tangu ilipotangazwa kuwa Jamhuri.

Katika kipindi hicho, taifa hilo limeongozwa na Marais watano, katika vipindi tofauti
December 12, 2024 at 10:28 AM
Rwanda yazindua maabara ya kupima ubora wa 'Helmet'
Rwanda imezindua maabara ya kwanza ya Kupima ubora wa'Helmet,’ inayolenga kuimarisha usalama barabarani na kuhakikisha viwango vya ubora wa kofia kwa waendesha pikipiki.
December 12, 2024 at 10:08 AM
Serikali ya Uturuki imeonyesha matumaini makubwa kufuatia makubaliano ya "kihistoria" yaliyofikiwa kati ya Somalia na Ethiopia katika mkutano uliofanyika Ankara.
December 12, 2024 at 9:55 AM
Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) kimetishia kutotoa leseni kwa mawakili wa Uganda. Hii inafuatia uamuzi wa Baraza la Sheria la Uganda kumnyima leseni ya muda mwanasheria wa Kenya Martha Karua. Karua alitaka kumwakilisha mwanasiasa wa Uganda Kiiza Besigye ambaye alikamatwa Kenya Novemba 2024.
December 11, 2024 at 2:07 PM
Zambia inafanya jitihada za kusuluhisha tatizo la malipo ya dola milioni 80 yaliyofanywa kimakosa na Shirika lake la Umeme, Zesco Ltd. kwa China wakati wa kukamilisha makubaliano kurekebisha deni na China.

Serikali imependekeza malipo hayo yatambulike kama malipo ya awali ya riba
December 11, 2024 at 10:23 AM