LULU za RAMADHAN.
banner
islamicamind.bsky.social
LULU za RAMADHAN.
@islamicamind.bsky.social
The influencer, optimistic and writer
"Tunawatakia waislamu wote ulimwenguni mfungo mwema wa mwezi wa ramadhani. Mwenyezi Mungu atupe afya njema, atukubalie ibada zetu na atusamehe makosa yetu. tukaweze kuzibadili nafsi na roho zetu kutoka kanuni pekee za aridhini kuelekea maadili ya mbinguni."
#Ramadhanikareem.
February 17, 2026 at 9:29 PM
Kufika kwa mwezi wa msamaha.
"Anasimulia Abuu Huraira (r.a) kuwa amesema Mtume (s.a.w) ibada ya swala tano, na kutoka ijumaa moja hadi nyingine, na kutoka ramadhani moja hadi nyingine ni sababu ya kufutiwa madhambi yaliyotendwa kati ya nyakati hizo pale ambapo madhambi makubwa yameepukwa."
February 16, 2026 at 4:31 PM
"Duniani hakuna uwezekano wa kuishi milele lakini kuna uwezekano wa kufanya ukumbukwe milele. Uwepo wetu tuufanye uwe sababu ya faraja kwa wengine. Afya, akili, elimu, mali na muda vyote hivi vinaweza kutufanya tukumbukwe milele endapo vitatumika katika njia sahihi."
February 15, 2026 at 8:46 AM
"انا للله وانا اليه راجعون.
#We are all belongs to Allah and to Him is our return."
February 11, 2026 at 8:09 AM
"Maisha yetu yana namna ya kujirudia. Ni kama sauti ya mwangwi unayoitoa kisha inajirudia. Lolote zuri au baya unalolifanya kwa mwingine lazima kuna siku litakurudia tu. Hata kama sio wewe atakuwa mwanao, hata kama sio mwanao basi atakuwa mjukuu wako. Tuwe wazuri ili wanaokuja pia wawe wazuri."
February 9, 2026 at 12:54 PM
"Binadamu ameweza kuogelea baharini kama samaki, ameweza kupaa angani kama ndege, lakini ameshindwa kutembea nchi kavu kwa uadilifu. Kadri teknolojia inavyozidi kukua ndivyo binadamu anavyozidi kupoteza utu wake"
February 9, 2026 at 8:48 AM
Wakati ulimwengu ukiwa kimya, Qur'an inakuwa ni ulimwengu unaosema na kuzungumza, inamtaka mwanadamu kufungua akili yake na fikra zake kwa mapana. kwa kuyahifadhi na kuyaelewa maudhui yake dunia inabaki salama, na wanadamu wanapata utukufu duniani na Akhera. #Qur'anmybook.
February 8, 2026 at 9:06 PM
February 7, 2026 at 6:51 PM
"You reap what you sow. Misfortune are your choice. By blaming you lose your power, and by complaining you scatter happiness." #theartoflife.
February 7, 2026 at 10:37 AM
"Na tazama baada ya mda wote huu, JUA halijawahi kuiambia DUNIA umenichosha!!. Angalia ni upendo wa namna gani huo, bado hueneza mwanga wake kote angani. Hadithi za mafanikio yetu zitasimuliwa kwa alfabeti za kuwahudumia wengine"
February 4, 2026 at 9:27 PM
"Tupo katika zama ambazo ndoa siyo tena jambo la heshima kwa mwanamke bali uwanja wa mapambano kati ya mwanaume na mwanamke. Ushindani huo unazidi kuenezwa, jambo pekee litakalo ondoa hali hii ni wao kurudi na kuishi kwa misingi ya Qur'an na sunna." #Kutokandoahadipeponi.
February 3, 2026 at 9:14 PM
Back to school. 2017 kwadelo sec. School.
February 3, 2026 at 5:53 PM
"Kuna utajiri mkubwa kuliko afya? Kuna furaha kubwa kuliko amani? Kuna neema kubwa kuliko uislamu? Kuna utukufu zaidi ya uchamungu?
Dunia hukosa thamani kwa mtu aliyeshindwa kupata haja ndogo. Kwa kukosa hekima na siri za baadhi ya mambo tunalalamika kwa vitu tulivyopaswa kushukuru"
February 2, 2026 at 7:53 AM
"Be a human or try to save humanity. Because of humanity our planet seem to be a safe place to live, otherwise there's no meaning of life." #free #palestine.
February 1, 2026 at 1:00 PM
"Moyo si wa kila mpitaji, ni amana. Na mapenzi bila taqwa ni safari ndefu isiyo na dira. Ewe nafsi yangu usinigeuke nikihitaji onyo, nikumbushe nikighafilika. Nahitaji mkweli pembeni yangu, nimechoka majaribu."
January 30, 2026 at 4:15 PM
"Katika hali yoyote ambayo Mwenyezi Mungu anatunyanyua sio tu ni kwa ajili yetu bali pia kwa ajili ya wengine. Tunapopitia njia ngumu ni ili tujenge kumbukumbu kuwa hayo ndiyo maisha ya wengine ya kila siku. Kwa kuwaangalia walioko chini yetu ndipo tunapoyapa maisha maana kamili."
January 29, 2026 at 6:50 PM
I think paradise will look like library.
January 29, 2026 at 1:08 PM
"Mwanamke anazidi kuwa mzuri zaidi kwa tabia njema, nafsi yenye kushukuru, moyo wenye kuridhika na jicho lisilo na tamaa. Kwa akili yake kubwa anakuwa amebeba dhima ya mwanamke halisi na nguzo tegemeo ya ulimwengu"
January 29, 2026 at 11:56 AM
"Ni asili ya mwanadamu kukata tamaa hasa pale anapokosa faraja na kutiwa moyo. Tunapokosa faraja kutoka kwa wengine tuna kimoja kilicho ndani yetu nayo ni IMANI kamwe tusiipoteze."
January 28, 2026 at 1:30 PM
"Miaka 100 ijayo dunia haitajali nilikuwa nani, niliishi wapi na niliishi maisha ya namna gani isipokuwa dunia itakuwa tofauti kwa sababu nilikuwa makini katika malezi ya mtoto."
January 26, 2026 at 6:09 PM
"Kila jambo huanzia kwenye ugumu kwenda kwenye wepesi. Bahati mbaya zaidi huwa hatujui ni sehemu gani huwa tumebakisha kufika katika kelele cha mafanikio pale tunapoanza kukata tamaa. Mafanikio makubwa hupatikana pindi subira inapovuka kiunzi cha majaribu"
January 24, 2026 at 5:21 PM
"Na wale wanaosema Mola wetu Mlezi tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamungu." 25:65
January 24, 2026 at 8:35 AM
"Ibada ya sala inatufundisha unyenyekevu na utii wa kiwango cha juu kwa Muumba wetu. Kuliweka chini paji la uso ambayo ni sehemu ya thamani na anayojivunia mwanadamu ni ishara ya kuwa pamoja na vyote anavyovimiliki mwanadamu bado ni dhalili mbele ya Mola wake."
January 23, 2026 at 10:13 AM
"Beyond the dry desert that you are crossing, you will find green pasture and fertile soil. The fruits therein grow profusely from all direction."
January 20, 2026 at 10:06 AM
Mola wetu tupe katika dunia mema na Akhera tupe mema na utukinge na adhabu ya moto. (al- Baqara)
January 16, 2026 at 6:53 AM